
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, Mhe. Onesmo Buswelu Mei 21 2025, amefanya ziara ya kukagua na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya awamu ya sita ikiwemo mradi wa utengenezaji wa madawati.
Akizungumza mbele ya hadhara akiwa kaongozana na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Ndg. Shabani Juma, DC Buswelu alibainisha kuwa jumla ya madawati 720 yatatolewa kwa shule nane za msingi wilayani hapo.

Mhe. Buswelu amesema shule ya msingi kungwi itapata mgao wa madawati 200, shule ya msingi Igunga itapata mgao wa madawati 150, shule ya msingi ilebula itapata mgao wa madawati 70, shule ya msingi kamsanga itapata mgao wa madawati 60, Shule ya msingi Mnyagala itapata mgao wa madawati 60, shule ya msingi Ntimba itapata mgao wa madawati 60, Shule ya msingi Kambanga itapata mgao wa madawati 60 na shule ya msingi Isilonge nayo itapata madawati 60.
Mara baada ya kusomewa mgawanyo wa madawati hayo katika shule za misingi 8 za wilaya ya Tanganyika, Mhe. Buswelu amefurahisha na kuridhishwa na utendaji kazi wa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa utengenezaji wa madawati hayo yaliyozingatia ubora yatakayomfanya mwanafunzi akae vizuri.
Mhe. Buswelu amesema kuwa kazi hiyo ni agizo kutoka Kwa Mhe. Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa mkoa wa Katavi Bi Mwanamvua Mrindoko yakuboresha mazingira mazuri ya kujifunzia Kwa watoto katika shule zote nchini.
Mwisho Mkuu wa wilaya ya Tanganyika, Mhe. Buswelu amewataka watoto wote kusoma kwa bidii kwani Mheshimiwa Rais yuko na Wanafunzi hao bega kwa bega kutatua changamoto zote.