Wanafunzi 11 wa darasa la 7 pamoja na mwalimu aliyekuwa anawafundisha katika Shule ya Msingi Uyole kata ya Kitwilu iliyopo kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wamenusurika kifo baada ya kupigwa na radi wakiwa darasani.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Omari Dendego, amefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa ambapo watoto hao wamefikishwa kwa ajili ya matibabu na kuwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari wakati huu mvua zikiendelea kunyesha.
Naye Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Dkt. Huruma Mwasipu amesema watoto hao wamepatwa na majeraha ya kuungua maeneo mbalimbali ya miili yao ikiwemo mikononi.