Na Eunice Kanumba – Shinyanga.
CHAMA cha mapinduzi (CCM) kimefungua rasimi pazia la wananchama kutia nia kugombea nafasi za ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi October mwaka huu, leo tarehe 28 june 2025 huku zoezi hilo likitarajiwa kufungwa tarehe 2 july 2025 saa kumi kamili jioni ambapo amewahimiza wanachama wote wa chama hicho kujitikeza kwa wingi kuchukua fomu ili washiri haki yao ya kuchaguliwa.
Miongoni mwa walijitokeza kutia nia katika jimbo la Shinyanga mjini ni mhandisi James Jumbe Wiswa ambapo amesema ametumia haki yake hiyo ya kikatiba kugombea jimbo hilo huku akigoma kuweka wazi mikakati aliyo nayo katika kulitumikia jimbo hilo akisema ni kunyume na kanuni na taratibu za chama cha mapinduzi huku akihaidi iwapo jina lake ritarejeshwa na chama na kuruhusiwa kufanya kampeni ataweka mikakati hiyo katika kuboresha jimbo la Shinyanga mjini.
“ Kwa kanuni na utaratibu wa chama huu sio muda wa kampeni nikitaja vipaumbele vyangu au nikisema kilichonisukuma ntakuwa navunja utaratibu kwa kuanza kampeni kabla ya wakati,kwa hiyo kwa hatua hii ya leo ni uchukuaji na urejeshaji wa fomu”amesema Jumbe

Mwingine aliyechukuaa fomu za kuwania kugombea nafasi hiyo ni mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni naibu waziri kazi ajira vijana na watu wenye ulemavu Patrobas Katambi akitaka kuomba ridhaa kwa awamu nyingine ya kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Lakini pia aliyekuwa mbunge wa Shinyanga mjini na makamu wa raisi wa bunge la Afrika (PAP) Stephen Masele amechukua fomu ya kugombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini kupitia chama hicho.

Naye mfanyabiashara maarufu mjini Shinyanga ambaye pia ni kada wa chama cha mapinduzi Gilitu Makula amejitosa kuchukua fomu ya kuwania ubunge katika jimbo hilo pamoja na kada mwingine wa chama cha mapinduiz aliyejukana kwa jina la Paul Joseph.
Jambo media imezungumza pia na katibu wa chama cha mapinduzi(CCM) wilaya ya Shinyanga mjini Hamisa Chacha ili kufahamu mchakato huo ambao leo ndo umeanza kwa siku ya kwanza ambapo amesema jumla ya wagombea watano wamejitokeza kuwania nafasi za ubunge katika jimbo hilo huku akisema mchakato huo bado unaendela hivyo wanachama wajitokeze kuchukua fomu hizo.

“Natoa wito kwa wanachama wote wa CCM kujitokeza kwa wingi kutia nia za kugombea nafasi za ubunge na udiwani ili washiriki haki yao ya kuchagua na kuchaguliwa “amesema Hamisa.
Kwa upande wa jimbo la Solwa mbunge wa jimbo hilo Ahmed Salum amechukua fomu ya kuendelea kulitumika jimbo hilo huku akiwashukuru wananchi wa Solwa kwa kuendelea kumuamini kwa muda murefu kuliongoza jimbo hilo, akiwataka kumpa ridhaa ya kuliongoza tena jimbo hilo endapo jina lake litafanikiwa kurejeshwa.

Mwingine aliyejitokeza kuchukua fomu ya kuwania jimbo hilo Jeremia Jilili ambapo ameomba dua za watanzania ili jina lake liweze kurejeshwa na chama ili aingie katika mchakato kwa mustakabali na ustawi wa jimbo la Solwa
Lakini pia kwa upande wa jimbo jipya la Itwangi, katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Shinyanga Richard Rafael Masele,amechukua fomu ya kuwania Ubunge katika Jimbo Jipya la Itwangi wilaya ya Shinyanga
“Leo nimechukua fomu ya kuwania Ubunge katika Jimbo Jipya la Itwangi,na ninasubili taratibu zingine za kichama na jina langu likirudi kati ya majina matatu nitazungumza zaidi,”amesema Masele.