WANACCM 128 WACHUKUA FOMU ZA UBUNGE KAGERA.

Jumla ya wanachama wa CCM 128 wakiwemo wabunge wanaomaliza muda wao katika Mkoa wa Kagera wamethibitishwa kuchukua fomu za kugombea nafasi ya ubunge katika majimbo yote 9 ya uchaguzi ya mkoa huo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Majimbo hayo ni pamoja na Bukoba Mjini, Bukoba Vijijini, Muleba Kaskazini, Muleba Kusini, Karagwe, Kyerwa, Ngara, Biharamulo pamoja na jimbo la Missenyi ambalo lilijulikana kama Jimbo la Nkenge.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa Kagera David Moleli amesema kuwa idadi hiyo imeonesha ongezeko la hamasa ya kisiasa miongoni mwa wananchi, hususan vijana na wanawake, waliojitokeza kwa wingi kutaka kuwania nafasi za uongozi.

Aidha Bwana David Moleli amesema kuwa maandalizi yote yanaendelea vizuri, huku akiwataka wagombea kuzingatia sheria, kanuni na maadili ya uchaguzi na kuwasisitiza kuendelea kuwa watulivu na kusubiri kufuata ratiba na mchakato ndani ya chama kwa utaratibu waliojiwekea ili kumpata mgombea wa chama atakayeipeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *