Wamiliki wa mabasi ya shule waandikiwa barua

Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani Jijini Dodoma limesema kuwa tayari limewaandikia barua wamiliki wa magari ya shule kuhakikisha wanayakagua na kuyafanyia ukarabati kabla ya shule kufunguliwa Januari 8,2024 ili kuondokana na ajali zisizo za lazima.

Hayo yamebainishwa na Koplo Ester Makali kutoka Ofisi ya mkuu wa kitengo cha usalama barabarani dawati la elimu kwa umma mkoa wa Dodoma wakati akizungumza na Jambo FM namna walivyojipanga kuhakikisha vyombo vya usafiri vinavyobeba wanafunzi vimekaguliwa kuelekea mwaka mpya wa masomo.

Sanjari na hilo ameongeza kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa madereva wa magari hayo kutokubali kupokea magari mabovu kutoka kwa wamiliki wa shule kwa kigezo cha ugumu wa Maisha kwani hali hiyo imekuwa ikiwasababishia wao kupata ajari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *