Walipewa madawa ya kulevya ili watulie

Imeelezwa kuwa raia wa Israel ambao walitekwa nyara na Hamas na kupelekwa Gaza walipewa madawa za kulevya ili kuwafanya wawe watulivu na wengine kudhulumiwa kingono, kulingana na daktari anayewatibu baadhi ya wale ambao wameachiliwa.

Renana Eitan, mkurugenzi wa kitengo cha magonjwa ya akili katika Kituo cha Matibabu cha Tel Aviv Sourasky-Ichilov, amesema unyanyasaji wa kimwili, kingono, kiakili, na kisaikolojia wa mateka walioachiwa huru ni mbaya sana.

Watoto walitenganishwa na familia zao, na mgonjwa mmoja alimwambia Eitan kwamba mateka kadhaa walikuwa wamezuiliwa kwenye giza kwa zaidi ya siku nne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *