Zaidi ya wanafunzi 20 waliorejeshwa masomoni mkoani Rukwa kupitia mfumo usio rasmi baada ya kukatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupata ujauzito wamelazimika kukatisha tena masomo kutokana na sababu zinazoshabihiana na zile za awali ikiwemo ujauzito.
Wanafunzi hao ni miongoni mwa wanafunzi 200 waliopata fursa ya kurejeshwa masomoni katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Rukwa.