Walionguliwa maduka Mwenge kukopeshwa

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameutaka uongozi wa Wilaya ya Kinondoni, kukutana na wafanyabiashara 32, ambao bishara zao zimeteketea, kufuatia moto uliotokea eneo la Mwenge, kuangalia namna ya kupata fedha za kuwakopesha.

Chalamila ametoa kauli hiyo leo, Jumanne Desemba 5, 2023 alipozungumza na wananchi baada ya kuwasili katika eneo la tukio.

“Uongozi wa Kinondoni ni muhimu kukaa na wafanyabiashara 32 ili kuangalia njia ya haraka na kama kuna fedha za kuwakopesha, wapewe ili walipe kwa riba kidogo,” amesema.

Kwa maoni yake, Chalamila anadhani kwamba japokuwa vyanzo vya moto katika maeneo kama hayo hutokea kwa bahati mbaya, lakini pia inaweza kuwa ni uhalifu ulioratibiwa au uzembe na hapa ndipo penye mantiki ya kuhitaji uchunguzi ufanyike.

Chalamila anataka uchunguzi huo ufanyike kwa muda mfupi ili kubaini chanzo cha moto huo, huku akisema kuwa kutokana na tukio hilo, imebainisha wazi ni kwa namna gani wafanyabiashara hawajui thamani ya benki.

“Wafanyabiashara wengi hawajui thamani ya benki kwani ndani ya moto kiasi kikubwa ya fedha kimeshuhudiwa kikiteketea,” amesema.

Kadhalika, ametaka uongozi wa wilaya hiyo, kujipa miezi sita kwa ajili ya ujenzi wa ene hilo ili kuepuka matukio kama hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *