Mashabiki waliolipa viingilio kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya TRA United na Simba SC ulioahirishwa awali kwa sababu ya mvua kesho wataingia bure.
Timu hizo za soka, zitamenyana kesho Aprili 9, 2026 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, baada ya mchezo wa awali kuahirishwa Machi 14, 2026.
