Waliogoma kusalimisha silaha kusakwa

Octoba 30 2023 Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime alitoa taarifa akieleza kuwa leo saa sita usiku itakuwa mwisho wa msamaha wa usalimishaji silaha na risasi haramu zinazomilikiwa bila kibali.

Jeshi hilo lilitangaza kuwa atakayekutwa anamiliki silaha kinyume cha sheria baada ya leo atafikishwa mahakamani na akitiwa hatiani atafungwa jela miaka 15.

Silaha hizo zinajumuisha ambazo wamiliki walifariki dunia na wanafamilia wakabaki nazo na wanapaswa kuzirejeshwa katika jeshi hilo.

Mwaka jana Jeshi la Polisi liliwashitaki wananchi 221 ambao hawakuitikia mwito wa kusalimisha silaha na wengine 17 kwa kosa la kumiliki risasi kinyume na sheria.

Masauni alihimiza wananchi ambao ndugu zao walikuwa wamiliki silaha kihalali na wakafariki dunia wazisalimishe silaha hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *