Idadi ya Wqtu waliofariki kutokana na tetemeko kubwa la ardhi nchini Myanmar imeongezeka na kufikia zaidi ya 1,000 na wengine 1,700 wakijeruhiwa.
Taarifa ya Serikali kitengo cha Maafa cha Nchi hiyo, kimeeleza kuwa Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 7.7 katika kipimo cha Richter lilipiga kaskazini magharibi mwa mji wa Sagaing Machi 28 na kusababisha uharibifu mkubwa.

Tayari hali ya hatari imetangazwa katika mikoa sita, ikiwa ni pamoja na Mandalay ambalo ni jiji la pili kwa ukubwa nchini humo, lililokuwa karibu na kitovu cha tetemeko.
Nayo ripoti ya kijeshi ya Myanmar imesema vifo 694 vimethibitishwa katika mkoa wa Mandalay pekee na kwamba watu 1,670 walijeruhiwa eneo hilo.