Watuhimiwa sita waliochoma Basi la Kampuni ya Saibaba wamefikishwa Kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Korogwe leo Machi 12, 2024 kwa ajili ya kusomewa shtaka lao linalowakabili.
Awali mwendesha Mashtaka wa mahakama ya Wilaya ya Korogwe Ndugu Sara Wangwe alibainisha kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo mnamo tarehe 27 Februari, 2024 katika eneo la Msambiazi Wilayani humo.
Nae Hakimu mkazi mwandamizi Flora Balijuye wakati akiwasomea shataka watuhumiwa hao la kuharibu mali chini ya kifungu cha sheria namba 326 cha kwanza cha kanuni ya adhabu, sura ya 16 iliyorejewa mwaka 2022 na kuwaeleza kuwa wanahaki kisheria ya kupewa dhamana ikiwa watakidhi masharti, na Kesi hiyo imehairishwa hadi tarehe 18 Machi, 2024 kwa ajili ya kusomewa hoja za awali.