Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Walimu wapigwa mapanga Bariadi, CWT walaani

Chama cha walimu tanzania (CWT) wilayani Bariadi kimelaani vikali tukio la mwalimu wa shule ya msingi Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu, ambaye amevamiwa na mtu asiyejulikana na kujeruhiwa kwa kukatwa mapanga usiku wa kuamkia Agosti 24, 2023.

Wakizungumza baada ya kufika nyumbani kwa mwalimu huyo baadhi ya viongozi hao wa CWT wamelaani kitendo hicho na kusema kuwa jamii inapaswa kuthamini michango ya walimu badala ya kuwafanyia vitendo viovu na vya kikatili.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyamagana Joseph Julius, amesema kuwa mwalimu huyo amejeruhiwa mikono yake yote miwili kwa kukatwa vidole kwa panga, huku akiiomba serikali isaidie kuimarisha ulinzi ili walimu wasiendelee kupatwa na matukio hayo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Simiyu Acp. Edith Swebe, amesema kuwa jeshi hilo limewakamata watu wawili wanaotuhumiwa kumjeruhi mwalimu huyo na kwamba uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea na watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *