Na Afarah Suleiman, Mbulu – Manyara.
Walimu wa shule za msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, wametakiwa kuongeza juhudi na ubunifu katika ufundishaji ili kuinua kiwango cha ufaulu wa wanafunzi, hususan katika shule zilizofanya vibaya katika matokeo ya Mtihani wa Taifa mwaka 2025 pamoja na upimaji wa kitaifa wa darasa la nne.
Akizungumza katika kikao cha Tathmini ya matokeo ya mitihani ya Taifa ya darasa la saba na upimaji wa kitaifa wa darasa la nne, Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Michael Semindu amesema, ni muhimu kwa walimu kutumia mbinu za ufundishaji kwa vitendo, ili kuongeza uelewa kwa wanafunzi juu ya masomo wanayofundishwa.

kwa upande wake, Afisa Elimu wa awali na msingi Wilayani Mbulu, Nicholaus Ngonyani, akitoa taarifa ya Tathmini hiyo, amesema ufaulu wa darasa la saba umeongezeka kwa asilimia 9.89, kutoka asilimia 71.56 mwaka 2024 hadi asilimia 81.45 mwaka 2025. huku ufaulu katika upimaji wa darasa la nne ukiongezeka kwa asilimia 3.1, kutoka asilimia 86.7 mwaka 2024 hadi asilimia 90.6 mwaka 2025.

Nao baadhi ya walimu walio walishiriki kikao hicho cha Tathmini walipopata nafasi ya kutoa mapendekezo na hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi, wamezitaja changamoto zinazofanya wanafuzi kuto kufanya vizuri ni mwamko wa elimu kwa wazazi pamoja na mazingira ya ni moja ya sababu ya mwalimu kufanya vizuri au kuto kufanya vizuri.



