
Walimu na waamuzi waliopatiwa mafunzo juu ya marekebisho ya sheria za mpira wa mikono (Handball) wametakiwa kuwa chachu katika kuibua vipaji vya wanafunzi katika shule za msingi na sekondari,katika kuendeleza suala zima la michezo kwani sekta hiyo kwa sasa imekuwa ikizalisha ajira nyingi.
Hayo yameelezwa na afisa elimu mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako wakati akifunga mafunzo ya awali ya waamuzi na walimu wa mpira wa mikono kwa shule za msingi na sekondari zilizopo mkoani Shinyanga yaliyofanyika katika shule ya Sekondari Uhuru mkoani humo.
Emmanuel Majura ni mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka chama cha mpira wa mikono ambaye pia ni mwenyekiti wakamisheni ya ufundi Tanzania amewaasa walimu waliopatiwa mafunzo kuyafanyia kazi ili fedha zilizotumika zisipotee bure.
Akielezea matarajio ya baadae yatakayotokana na mafunzo hayo afisa maendeleo ya michezo mkoa wa Shianyanga Jesca Simchile amesema mafunzo hayo yatasaidia kutengeneza timu imara itakayo fanya vizuri katik mashindano ya mkoa na kitaifa na hatimaye kupata wachezaji watakaoshiriki michuano ya Afrika Mashariki mwaka 2025
Aidha walimu waliopatiwa mafunzo hayo wamekishukuru chama cha mpira wa mikono katika mkoa wa Shinyanga kwa kufanikisha upatikanaji wa elimu hiyo,kwani itakwenda kuamsha ari ya michezo katika mkoa huo na kwamba wamepata mwanga wa kuendesha michezo hiyo tofauti na awali ambapo hawakufahamu mabadiliko ya sharia za mchezo huo.