WALEMAVU KUNDI MAALUM WAJENGEWA UWEZO MASUALA YA AFYA YA UZAZI

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

Serikali kwa kushirikiana na shirika la World Vision Tanzania kupita mradi wa GrowEnrich, imeendesha mafunzo ya siku mbili kwa kundi Maalumu la Walemavu, ili kuwajengea uwezo katika masuala ya afya ya uzazi, ukatili wa kijinsia, malezi na makuzi pamoja na elimu kuhusiana na ugonjwa wa ukimwi, yaliyofanyika katika ukumbi wa Katemi uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga, Lyidia Kwesigabo amesema lengo hasa la kuendesha mafunzo hayo kwa kundi hilo ni kuwawezesha kukabiliana na changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na  unyanyapaa wanaofanyiwa walemavu hususan katika masuala ya uzazi.

“Serikali ya mkoa kwa kushiriakiana na shirika la  World Vision Tanzania Tumeamua kuwajengea uwezo kundi la walemavu kutoka halimashuri tatu za mkoa wa Shunyanga ambazo hi halimashauri ya wilaya ya Shinyanga Kishapu na Shinyanga manispaa ili waweze kuwa na uelewa juu ya masuala ya afya ya uzazi,lishe malezi na makuzi pamoja uelewa wa aina mbalibali za ukatili wa kijinsia,” amesema Kwesiagabo.

Naye meneja  mradi wa Grownrich unaoratibiwa na shirika la world vision Tanzania ambao unaoshughulika na afya ya uzazi, lishe malezi na makuzi  Shukran Dickson amesema kuwa na ulemavu sio sababu ya binadamu yeyote aliyeumbwa na mweyezi Mungu kukosa thamani na haki za msingi  huku akiwataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa chachu kwa wengine ambao hawakufanikiwa kufika katika mafunzo hayo ili wakatambue haki na thamani zao.

“Sisi kama world Vision kuptia mafunzo haya tumetengeneza askari wa kusaidia walemavu wote kupata haki zao”amesema Shukran

Naye Afisa Mradi wa Grownrich unaoshughulika na afya ya uzazi malezi na makuzi kutoka world vision Tanzania, JohnSton Mwesiga amelezea malengo ya taasisi hiyo katika kuwafikia watu wenye ulemavu na kuwajengea uwezo kielimu huku akiweka wazi takwimu juu ya watu wenye ulemavu waliowafikia mpaka sasa .

“Katika utekelezaji wa shughuli zetu ambapo tupo katika mwaka wa tatu wa utekelezaji lengo likiwa baada ya miaka mitano ifikapo 2027 kuwafikia watu wenye ulemavu Zaidi ya mia tisa”amesema Mwesiga

Akitoa hotuba ya kufunga mafunzo hayo mganga mkuu mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile amesema serikali inalitambua kundi hilo muhimu na imekuwa ikirishikisha katika mipango mbalimbali ya  ustawi na maendeleo kwa  kundi hilo na kwamba mafunzo hayo ni maelekezo ya serikali kutoa elimu hiyo ususani katika eneo la ukatili.

Nao baadhi ya washiriki wameishuru serikali  kwa kushikiana na World Vision Tanzania  kuwapatia mafunzo hayo ambapo wamekiri kuwa elimu hyo  ilikuwa bado haijawafikia huku wakieleza pia changamoto ya mawasiliano katika baadhi ya maeneo hususan katika vituo vya afya inavyowasumbua pindi wafikapo  kupata huduma na kushauri  wapewe kipaumbele wafika katika  maeneo hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *