
Baadhi ya wananchi mkoani Shinyanga wamelalamikia ungezeko la nauli za mabasi ya masafa marefu zilizoanza kutumika rasmi leo decemba 8, 2023 kwa mujibu wa mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA).
Wakizungumza na Jambo FM wananchi hao wamesema kuwa changamoto kwao ni ugumu wa maisha ambao unawafanya kushindwa kumudu baadhi ya mahitaji muhimu ikiwemo ongezeko hilo la nauli.
Malalamiko hayo yanakuja mara baada ya latra kutangaza kuanza kutumika rasmi kwa nauli za mabasi ya masafa marefu na mafupi kuanza kutekelezwa rasmi leo ljumaa.
Itakumbukwa November 27,2023 LATRA ilitangaza ongezeko la nauli kwa mabasi ya mjini ya masafa mafupi na mabasi ya safari za masafa marefu baada ya kupitia maoni ya wadau wa usafiri nchini.