WAKUU WA WILAYA WATUMIKIENI WANANCHI – RC PAUL CHACHA.

Mkuu wa mkoa wa Tabora Paul Chacha amewataka wakuu wapya wa wilaya za Tabora mjini na Sikonge kufanya kazi kwa bidii na kuwatumikia wananchi ipasavyo na kutatua kero zao.

Mhe. Paul Chacha ametoa maagizo hayo wakati wa hafla ya kuwaapisha viongozi hao wapya ambao ni mkuu wa wilaya ya Tabora Mhe. Upendo Wella na mkuu wa wilaya ya Sikonge Mhe. Thomas Mnyinga.

“Mafanikio tulionayo ni kwa sababu ya uchapakazi, mkienda mtakuta watu ofisini wapo, mkafanye kazi kwa ushirikiano na na kila mtu katika maneno yenu. Ukitaka kufeli utakuwa umejitakia wewe mwenyewe.” Amesema Chacha.

Pia RC Chacha amewaagiza watumishi wa umma mkoani Tabora kuwasikiliza na kuwahudumia wote wanaofika ofisini kwao kwa unyenyekevu.

“Jamii zetu za kitanzania tunazifahamu, unajua mtumishi au mwananchi akifika ofisini kwa afisa utumishi halafu shida yake haishughulikiwa kwa sababu ya mtu mmoja tu ambaye hawajibiki, huyo mwananchi atawachukia wote kuanzia mkurugenzi wa halmashauri mpaka mkuu wa wilaya, kumbe ni tatizo tu la mtu Mmoja mzembe.” Amesisitiza Chacha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *