Wakutwa wamefariki mgahawani bila nguo

Mwanamke mmoja aitwa Swiga John Mwakalobo na Mwanaume ambaye amefahamika kwa jina la Jacob Chang’a Wakazi wa Kata ya Mkwawa Wilaya na Mkoa wa Iringa wamekutwa wamefariki katika mgahawa huku wakiwa hawajavaa nguo.

Ndugu na Majirani wamesema marehemu Swiga hadi usiku alikuwa akiendelea na shughuli zake za mgahawa na huwa anachelewa kufunga kutokana na maandilizi ya chakula cha asubuhi .

Wameongeza kuwa Hadi imefika asubuhi hawakumuona Swiga, ndipo wakafanya juhudi za kumtafuta kwa kumpigia simu Mume wake bila mafanikio ya kumpata na hata simu yake ilikuwa haipokelewi ndipo wakaenda mgahawani kwake na kupiga simu na kusikia inaita ndani huku mlango umefungwa na baada ya kuchungulia walikuta miili miwili iko ndani ambayo ilikuwa uchi, wakavunja mlango.

Mwenyekiti wa Mtaa huo wa Imalanongwa A. Hamis Chananja amethibitisha kutokea kwa kwa tukio hilo katika eneo lake na amesema Polisi wamefika kuchukua miili hiyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *