Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wakulima wa nanasi Geita walia na soko la uhakika

Wakulima wa zao la Nanasi Mkoani Geita walia na soko la uhakika la zao hilo
Wakulima wa zao la Nanasi katika vijiji vya Sungusira na Igate kata ya Nzera wilayani Geita Mkoani Geita wamelalamikia Changamoto ya ukosefu wa soko la uhakika la zao hilo licha ya kuzalisha kwa wingi hali inayopelekea wananchi kushindwa kunufaika na zao hilo hivyo wameiomba serikali kuwajengea kiwanda cha kuchakata zao hilo ili kuongeza thamani.


Wamebainisha hayo wakati wakizungumza na Jambo Fm kwa nyakati tofauti ambapo wamesema kwa sasa wanalazimika kuuza nanasi 5 kwa kiasi cha Shilingi 1,500 huku wakiwa hawana wateja wa uhakika hali ambayo inapelekea kuharibika kwa bidhaa hiyo nakujikuta wanapata hasara kubwa ambapo wameiomba serikali kuwajengea kiwanda kidogo katika maeno yao ili kupata soko la uhakika na kunusuru mazao yao kuharibika kila wakati.

Mwenyekiti wa umoja wa wakulima wa nanasi na wafanyabiashara katika vijiji hivyo Nyasuka Nyamhanga amesema kilimo cha nanasi kimegeuka mzigo kwa wananchi kutokana na kutumia gharama kubwa wakati wa kilimo lakini wakiivisha hakuna soko la uhakika hali ambayo inawalazimu kuwakopesha wanunuzi wachache wanaojitokeza ili kunusuru mazao yao.

Aidha Katibu Tawala Msaidizi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita anayeshugulikia masuala ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Chacha amesema ili kunusuru zao hilo serikali ipo kwenye mchakato wa kutafuta mwekezaji ili kujenga kiwanda cha kutengeneza mvinyo wa zao hilo hali itawarahisishia wakulima kupata soko la uhakika na bei elekezi ili waweze kunufaika na zao hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *