Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wakulima wa Dengu  Nyang’wale Wagomea Bei ya 1610 Kwa Kilo

Costantine James,Geita

Wakulima wa zao la dengu wilayani Nyang’wale Mkoani Geita Wamegoma Kuuza Zao hilo kwa bei ya shilingi 1,610 kwa kila kilo kupitia mfumo wa Stakabadhi ghalani wakitaka kuuza kwa shilingi elfu 2,000 kwa kila kilo wakisema bei hiyo ya madalali inawanyonya na kuwapa hasara kubwa kutokana na kutumia gharama kubwa katika uzalishaji wa zao hilo.

Wakizungumza katika mnada wa zao hilo baadhi ya wakulima wa zao hilo wamesema kutokana na bei kutokuwa rafiki kwao wamelazimika kutokuuza mazao yao ili kuepuka hasala inayoweza kujitokeza nakuiomba serikali kusimamia vyema bei kupitia mfumo wa Stakabadhi ghalani ili iweze kuleta manufaa kwa wakulima.

Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika Mkoa wa Geita Zainabu Mahenge amesema bei waliyoitoa madalali kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani haileti tija kwa wakulima hali iliyopelekea kusitishwa kwa mnada wa zao hilo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Geita, Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale,Grace Kingalame amefika katika mnada huo na kutoa maagizo ya kuahirishwa kwa mnada huo ili kutafuta bei ambayo itawanufaisha wakulima wa zao hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *