Na Afarah Suleiman Hanang’ – Manyara.
Jumla ya Wakulima 20 Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara wamepatiwa mkopo wa vifaa vya kilimo, ikiwemo Trekta kutoka kampuni ya Pass Leasing yenye thamani ya shilingi Bilion 1.4.
Akizungumza na Wakulima pamoja na Wananchi waliojitokeza kwenye hafla ya ukabidhiwaji Matreka hayo, Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Halmishi Hazal amewataka wanufaika wa mikopo hiyo ya matrekta kuhakikisha wanaendela kuongeza tija kwenye kilimo ili kunufaika zaidi ,ikiwa pamoja na kurudisha mikopo hiyo kwa wakati.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Pass Leasing Nchini, Killo Lusewa amesema mpaka sasa Kampuni hiyo imeshatoa vifaa vya Kilimo vyenye thamani ya Bilion 70 tangu kampuni hiyo izaliwe kutoka kwa Kampuni tanzu ya Pass Trust.
Aidha miongoni mwa wakulima waliopata mkopo wa Trekta na mgombea udiwan wa kata ya Gitting Marko Mamoya ameishukuru kampuni ya Pass Leasing na kusema sasa ataenda kuongeza ukubwa wa maeneo ya kilimo kutoka Ekari 30 alinazolima sasa ili kuongeza tija kwenye kilimo hicho.




