Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wakishindwa kulipa mikopo wanalipa ngono

Imeelezwa kuwa suala la marejesho ya mikopo umiza ni moja ya chanzo kinachopelekea matukio ya ukatili wa kingono kwa baadhi ya wanawake hapa nchini hii ni kutokana na baadhi ya wanawake hao kushindwa kulipa mikopo hiyo kwa wakati.

Hayo yameelezwa na kaimu jaji mfawidhi wa mahakama kuu ya kanda ya Mwanza Stanley Kamana wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga maatukio ya ukatili wa kijinsia mkoani humo, ambapo amesema baadhi ya wanawake wamekuwa wakinyanyaswa kijinsia kwa sababu ya kutafuta marejesho ya mikopo umiza hivyo kuna haja ya serikali kupitia watunga sera waandae mfumo wa utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu ili wanawake waweze kujiinua kiuchumi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za wanawake na watoto (kivulini) Yassin Ally amesema kwa siku za hivi karibuni matukio ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kwa mikoa ya kanda ya ziwa kwa kiasi fulani yameanza kupungua kwani kwa mujibu wa takwimu za taasisi ya taifa iliyotolewa mwaka 2022 inaonyesha matukio hayo yamepungua kwa kiasi kikubwa, akitolea mfano mkoa wa Shinyanga hapo awali ulikuwa na asilimia 78 ila umepungua mpaka asilimia 38 huku mkoa wa Mwanza ukipunguza matukio hayo kutoka asilimia 60 mpaka asilimia 47.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *