Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wakazi Wa Kata Ya Nyatwali Wilayani Bunda Mkoani Mara Waondokana Na Uvamizi Wa Wanyama Wakali.

Na Adam Msafiri

Wakazi wa kata ya Nyatwali wilayani Bunda mkoani Mara wameishukuru serikali kwa kuwalipa fidia na kuwahamisha katika kata hiyo ambayo ilikuwa na matukio ya mara kwa mara ya uvamizi wa makundi ya wanyama hatari kama vile tembo na kuwasababishia hofu juu ya usalama wao

Mary Wambura na Sayida Jilala ambao ni miongoni mwa waliokuwa wakazi wa eneo hilo la Nyatwali,wamesema imekua ni ngumu kwao kufanya shughuli za maendeleo katika eneo hilo,kwani mazao huishia kuliwa na Tembo na kusababisha adha ya kukosa chakula.

‘Kitu kingine ambacho tulitakiwa kujua sisi kama Watanzania,serikali ilikua ina uwezo wa kutuhamisha hata bila malipo kwa sababu ardhi ni mali ya Tanzania,lakini kwa huruma ya serikali wameamua kutuhamisha na kutupa fidia ili tuweze kupata kianzio tunakokwenda kwahiyo tunaishukuru sana’Amesema Bi Mary Wambura.

Kwa upande wake Kamishna msaidizi wa uhifadhi kutoka Tanapa anayeshulikia migogoro ya mipaka ya hifadhi Kamishna Mathew Mombo amesema tayari serikali imewalipa watu 2,888 kati ya watu 4,112 wanaotarajiwa kulipwa fidia huku idadi iliyobaki ni ndogo na zoezi la ulipaji linaendelea.

Aidha Mathew ameongeza kuwa Nyatwali ni eneo kubwa ambalo litakuwa na manufaa makubwa katika uhifadhi lakini pia ni eneo ambalo litasaidia sana wanyama hawa kuwa na sehemu ya kupita kwa urahisi kwenda kupata maji katika Ziwa Victoria,na watu ambao wamekwisha kupewa fidia mpaka sasa ni watu 2,888′.

Hata hivyo serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vincent Naano ameeleza kuwa eneo hilo linatwaliwa kutoka kwa wananchi ili kupisha mapitio ya wanyama kutoka hifadhi ya Taifa ya Serengeti kuelekea Ziwa victoria kwa ajili ya kupata maji.

‘Sisi serikali tunawashukuru sana wananchi wa Nyatwali kwa uamuzi huu wa wao kuhama na wamefurahia kwa sababu kwa adha wanayopata kila mwaka ya wanyama wakilima Tembo wanatafuna,wakihifadhi kwenye maghala Tembo wanavunja nyumba na kwa kipindi hiki wakiwa wanahama basi tutazidisha ulinzi kwa wananchi ili kuzuia wanyama hawa’Ameeleza Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vincent Naano.

Kiasi cha shilingi bilioni 45 zitatolewa na serikali kama fidia kwa wakazi wa mitaa ya Kariakoo,Serengeti,Tamau na Nyatwali ambao baadhi yao tayari wamekwisha kuanza kuondoka katika eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *