Wakandarasi,Wazabuni Wanaodai Shinyanga Manispaa Hawajasahaulika

Na Eunice Kanumba,Shinyanga MC

Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imeahidi kulipa madeni yote ya huduma za wazabuni pamoja na wakandarasi walizozitoa katika halimashuri hiyo kupitia miradi mbalimbali iliyotekelezwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 ulioisha tarehe 30 Juni mwaka huu.

Muweka wa hazina wa halmashuri ya manispaa hiyo Mulokozi Kishenyi ameeleza hayo alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze katika kikao maalumu cha baraza la madiwani kilichoketi kujadili taarifa za hesabu za mapato na matumizi ya halmashauri hiyo Agosti 29,2024 ambapo amesema halmashauri hiyo inatarajia kukamilisha madeni yote katika bajeti ya mwaka wa fedha ulioanza tarehe 1 Julai 2024.

Awali akiwasilisha hoja yake katika mkutano huo Diwani wa kata ya Mwawaza Juma Nkwabi amesema haoni sababu ya watoa huduma katika halimashuri hiyo kucheleweshwa kupewa haki yao wakati walitumia mitaji yao kukamilisha miradi mbalimbali na malipo yao hadi sasa kuwekwa katika akaunti ya amana wakisubiri ukamilishaji wa miradi.

Akifunga kikao hicho Mstahiki Meya wa Halimashuri ya Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko amehimiza ulipaji wa madeni hayo na kuwapongeza madiwani wa Halmashauri ya Manispaa hiyo kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato kutoka shilingi bilioni 2 kwa mwaka 2020 hadi shilingi bilioni 5 kwa mwaka huu pasipo kuongeza kodi kwa wananchi wala chanzo cha mapato.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *