WAISLAMU WAHIMIZWA MATENDO MEMA, KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU

Na Saulo Stephen – Singida.

Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Kata ya Mandewa Mkoani Singida, wametakiwa kushehekea Sikukuu ya Eid Al Adha kwa kuitunza amani ya nchi iliyopo ikiwa ni pamoja na kutenda matendo yaliyomema sanjari na kushiriki uchaguzi mkuu wa 2025 kwa amani na utulivu.

Hayo yameelezwa na Imamu wa msikiti wa Unyakumi uliopo mjini Singida Shekh Omari Hamisi Missanga wakati akitoa mawaidha kwenye swala ya Eid El Adha iliyofanyika katika viwanja vya Msikiti wa Unyakumi, ambapo amewaasa waumini hao kuhakikisha wanakuwa mfano wa kuigwa katika jamii kwa kutenda matendo yanayompendeza mwenyezi Mungu vilevile yanayohubiri Amani ili kuilinda amani ya Nchi.

Aidha Imamu Missanga pia amewataka waumini hao kujiandaa kikamilifu katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025 kwa kuwataka kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo pamoja na kusimamia Amani iliyopo kuanzia ngazi za chini mpaka ngazi za juu za uongozi pindi muda wa kupiga kura kuwachagua viongozi utakapowadia.

Pamoja na mambo mengine pia amewataka waislamu kutumia siku hii ya Eid Al Adha kwa kusherehekea kwa amani ikiwa ni pamoja na kuchinja wanyama walioruhusiwa kwa mujibu wa siku hii,sanjari na kushiriki nyama hiyo na watu ambao hawajajaaliwa kuchinja katika sikukuu hii.

Nao baadhi ya waumini wa Kiislamu wakizungumza na jambo fm katika viwanja vya Mskiti Unyakumi wamesema sikuu hii ni muhimu kwao kwani wanaisherehekea kwa amani na upendo ikiwa ni pamoja na kuchinja vilivyohalali kama inavyoelekeza misingi ya dini hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *