WAHITIMU KIDATO CHA SITA SOLYA WAFUNDWA MISINGI YA KUJITEGEMEA

Na Saulo Stephen – Singida.

Wahitimu wa kwanza wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Solya iliyopo Wilayani Manyoni mkoani Singida, wameaswa kujenga misingi ya kujitegemea, nidhamu na maadili bora ili kuwa rasilimali yenye tija kwa taifa.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Katibu Tawala wa Mkoa, Dkt. Fatuma Mganga, amewapongeza wahitimu 182 na kuwataka kutumia elimu waliyoipata kujijenga kiuchumi na kijamii na kiwasisitiza wasipende utegemezi bali wakajifunze kujitegemea na kutumia fursa zilizopo mitaani.

Aidha amewasisitiza umuhimu wa kujiepusha na vitendo hatarishi kama matumizi ya dawa za kulevya na mimba za utotoni, akihimiza matumizi sahihi ya teknolojia kwa maendeleo na kujifunza ujasiriamali.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Dkt. Vincent Mashinji amesema serikali inalenga kujenga kizazi chenye mchango chanya kwa kutengeneza kizazi chenye faida kubwa kwa taifa.

Nao Wahitimu wameishukuru serikali kwa fursa ya elimu na kuahidi kufanya vizuri katika mitihani yao, huku wazazi wakisisitiza nidhamu na ushirikiano katika malezi.

Solya Sekondari iliyoanzishwa mwaka 2024 sasa ina zaidi ya wanafunzi 700 kutoka 84 wa awali, ikiwa ni matokeo ya uwekezaji wa serikali katika elimu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *