WAHITIMU KIDATO CHA SITA MANYARA GIRLS WAHIMIZWA UADILIFU KUZIFIKIA NDOTO ZAO

Na Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Wahitimu wa kidato cha sita katika shule ya Sekondari ya Wasichana Manyara (Manyara girls) watakiwa kuwa waadilifu na kujilinda, ili kufikia ndoto zao na kutumia maarifa waliyoyapata, ili kuleta maendeleo kwa taifa, mara baada ya kuhitimu masomo yako.

Wito huo, umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Fakii Lulandala wakati akitoa hutuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga katika mahafali ya kwanza ya kihistoria ya kidato cha sita katika Shule ya Wasichana Manyara.

“Tumieni maarifa na ujuzi mlioupata hapa shuleni ili kutimiza ndoto zenu na kuleta maendeleo katika jamii,” alisema Lulandala.

Awali akisoma Taarifa ya Shule Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Gizela Msofe ameiomba Serikali kuwajengea kichomea taka, pamoja na kuwekwa kwa uzio wa shule hiyo.

Akiongea kwa niaba ya wazazi wa wahitimu wa kidato cha sita, mmoja wa wazazi hao amewashukuru walimu kwa Elimu ambayo wameitoa kwa watoto wao, na kuwataka wazizi ambao watoto wao bado wapo shuleni kushirikiana na walimu, ili kupata ufaulu mzuri kwa wanafunzi.

Nao baadhi ya wahitimu, wamesema watakwenda kusimamia maadili katika kupamba na vikwazo watakavyokutana navyo mtaani kwa kutumia ujuzi na elimu waliyoipata kwa kipindi cha miaka miwili wakiwa shuleni hapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *