Hospitali ya Benjamin Mkapa inakabiliwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa figo ambapo kwa siku watu zaidi ya 50 husafishwa damu.
Kutokana na hali hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dk Alphonce Chandika, amewashauri wananchi kuzingatia mtindo bora wa maisha ili kulinda figo zao.
“Watu wenye tatizo la figo wanasafisha damu mara tatu kwa wiki, wananchi wanapaswa wafanye mazoezi kuzingatia mlo usioathiri moyo ili kuzilinda figo zao, ” amesema.
Pia, amesema wananchi wanapaswa wafanye mazoezi na kuzingatia mlo kamili usioathiri moyo ili kuzilinda figo.