Waganga wa jadi chanzo cha wajawazito kutofika Kliniki

Imeelezwa kuwa licha ya serikali kuweka vituo vingi vya kutolea huduma za afya, bado kuna idadi ndogo ya akina mama wajawazito ambao hawahudhurii kliniki na wakati wa kujifungua wanajifungulia nyumbani jambo ambalo linahatarisha maisha yao na watoto wao.

Hayo yamesemwa na mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Itilima dk. Emmanuel Costantine wakati akizungumza na Jambo Fm ofisini kwake na kueleza kuwa wanawake wengi wanaojifungulia nyumbani mara nyingi huvuja damu nyingi na hata kupoteza maisha wakiwa nyumbani bila kupata huduma ambayo wangeipata katika kituo cha kutolea huduma za afya.

Dk. Costantine amesema kuwa moja ya sababu ya wanawake kutowahi kliniki wilayani humo ni kutokana na uwepo wa waganga wengi wa tiba asili na wakunga wa jadi ambapo wanawake wanapopata dalili za ujauzito huenda kutibiwa kwao na kujikuta wanachelewa kuanza kliniki.

Mwenyekiti wa waganga wa tiba asili wilayani itilima shija lugalila limbe, ameeleza namna ambavyo wanawasaidia kuwaushari akina mama wajawazito kwenda katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Baadhi ya wakazi wa bariadi wameeleza faida za kuhudhuria kliniki wakati wa ujauzito na kuwaasa wanawake kuachana na mazoea ya kwenda kwa waganga wa tiba asili kipindi cha ujauzito kwani huko hawawezi kupata vipimo vyovyote vya kitaalam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *