Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wafukua kaburi na kuondoka na Sanda

Katika hali isiyo ya kawaida mwili wa kijana Idd Salum anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 22, uliozikwa siku ya Jumatano Octoba 11 2023 katika makaburi ya waislam mtaa wa Nyahingi kata ya Mkolani Jijini Mwanza umekutwa umefukuliwa na watu wasiojulikana na kuondoka na sanda ya marehemu.

Akizungumia tukio hilo mwenyekiti wa mtaa wa Nyahingi Korneli Mwakabenga amesema mwili wa kijana huyu ulizikwa na baada ya maziko kufanyika kila mtu alitawanyika ila asubuhi ya Octoba 12 2023 alipokea taarifa kutoka wananchi walio karibu na makaburi hayo wakimtaarifu kuwa mwili umefukuliwa ndipo alipofika na kukuta tukio hilo kweli limetokea.

Kwa upande wake kiongozi wa msikiti wa Khayrudini uliopo katika eneo la Mkolani Said Mselem, amesema baadhi ya watu walikwenda katika makaburi hayo kwa ajili ya kufanya swala ila cha kushangaza walikuta mwili huo ukiwa umefukuliwa huku sanda ya marehemu ikiwa haipo. Nae kaka wa marehemu alifahamika kwa jina la Salim Kulwa amesema wao kama familia wanasikitishwa na tukio hilo ambapo wanalihusisha na imani za kishirikina kwani mpaka wanazika mwili wa marehemu sanda ilikwepo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *