Baadhi ya wafanyakazi wa Jambo Fm leo Octoba 18 2023 wametembelea Jambo Bakery ili kujionea utengenezaji wa bidhaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na mkate wa nazi uliozinduliwa hivi karibuni.
Bidhaa nyingine zinazotengenezwa na Jambo Bakery ni pamoja na maadazi, keki, mkate wa maziwa , na mkate wa kawaida, ambapo kwa siku hutengenezwa Zaidi ya mikate 22,000 kwa siku.
Wateja wakubwa wa bidhaa hizi ni wa mikoa jirani ya kanda ya ziwa ikiwemo Tabora, Mwanza, Kagera , Mara , Geita na hivi karibuni bidhaa hizi zitaanza kupatikana nchi nzima pamoja na nchi jirani kama vile Burundi, Uganda, na Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo.
Octoba 13 2023 Jambo Bakery ilizindua bidhaa mpya ya mkate wa nazi ambao umepokelewa vyema sokoni ,na unapatikana madukani kwa bei ya shilingi 1,500 kwa Mkate mdogo na shilingi 4,000 kwa mkate mkubwa.