WAFANYAKAZI SERIKALI INAWASIKILIZA, INAWATHAMINI CHAPENI KAZI – RAIS SAMIA

Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, amewataka wafanyakazi nchini kuchapa kazi na kwamba Serikali ipo inawasikiliza na kuwathamini.

Amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kazi na maslahi ya watumishi kadri uchumi utakavyoruhusu. Pia Serikali itaendelea kuchukua hatua zaidi za kuimarisha ustawi wa wafanyakazi.

Dkt Samia ameeleza leo Ijumaa Mei Mosi,2026 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ‘Mei Mosi’, yaliyofanyika kitaifa mkoani Njombe.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono Wafanyakazi waliokuwa wakipita mbele ya Jukwaa Kuu katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi 2026), ambayo Kitaifa yamefanyika leo Mkoani Njombe.

“Ndugu zangu chapeni kazi Serikali ipo, inawasilikiza inawathamini,” amesema na kuongeza kuwa:

“Sote kwa pamoja hatuna budi kushirikiana, kuamianiana na kutanguliza maslahi ya Taifa letu, ninawahimiza tuendelea kufanya kazi kwa bidi, kwa uadilifu na weledi ili kujenga uchumi na ustawi wa jamii,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *