WAFANYABIASHARA WASIOTOA RISITI WAKALIA KUTI KAVU

Mkuu wa mMkoawa Manyara, Queen Sendiga amewaonya baadhi Wafanyabiashara wasiotoa au kutoa risiti ambazo haziendani na thamani ya mauzo, hali inayokwamisha zoezi la ukusanyaji wa kodi.

Sendiga ameyasema hayo hii leo Februari 20, 2025 katika kilele cha siku ya mlipa kodi ambacho kimeambatana na pongezi kwa walipa kodi.

Amesema, kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa sio wazalendo kwa kufanya udanganyifu wanapotembelewa na maafisa wa tra ambapo ameitaka jamii kutoa taarifa wanapowaona Wafanyabiashara wa namna hiyo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Kamishna wa TRA Nchini, Hashim Ngoda amesema mamlaka hiyo inashirikiana na Wafanyabiashara kuhakikisha inalinda biashara zao na wameunda timu maalum inayowatembelea kwenye maeneo yao na kutoa elimu kuhusu ulipaji kodi.

Awali, Meneja wa TRA Mkoa wa Manyara, Alex Katundu amesema wamevuka lengo la ukusanyaji wa kodi kutokana na elimu ambayo wamekuwa wakiitoa kwa Wananchi kuhusu umuhimu wa ulipaji wa kodi ambazo pia zimesaidia kuleta maendeleo ikiwemo sekta ya Maji, Afya, Elimu n.k.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *