Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wafanyabiashara wa soko la Mabatini Jijini Mwanza walia na miundombinu mibovu

Wafanyabiashara wa soko la Mabatini lililopo wilaya ya Nyamagana mkoa wa Mwanza wamelalamikia ubovu wa miundombinu iliyopo katika soko hilo hali ambayo imesababisha wafanyabiashara kuhama na kwenda kufanya biashara nje ya soko ili kuwafuata wateja wasioweza kuingia ndani ya soko.

Wakizungumza na Jambo FM baadhi ya wafanyabiashara hao wamesema hali ya miundombinu iliyopo katika soko hilo sio ya kuridhisha na imekua ikiwaathiri sana hususani kipindi cha mvua kutokana na maji ambayo hutuama na kusababisha kuoza kwa bidhaa zao licha ya kuwakosesha nafasi ya kupita wanunuzi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa soko hilo Bakari Rajabu amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na ameiomba serikali iweze kufanya maboresho ya haraka katika soko hilo ili kuwanusuru na changamoto hiyo.

Jambo FM imemtafuta afisa biashara wa jiji la Mwanza Madelina Mtweve ambae amesema kwa mwaka wa fedha 2024/2025 tayari halmashauri ya jiji la Mwanza tayari imetenga bajeti ya kufanya maboresho ya miundombinu katika masoko mbalimbali ya jiji hilo likiwemo soko la Mabatini ili yaweze kusaidia kupanua wigo wa mapato kwa jiji la Mwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *