Wachungaji wanakodi watu kutoa ushuhuda wa uongo

Wananchi wa wilaya ya Sengerema Jijini Mwanza wameiomba serikali iweze kuwachukulia hatua wachungaji feki waliopo katika wilaya hiyo kwani kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakiipotosha jamii.

Rai hiyo imetolewa na wananchi hao wakati wakiwa katika mkutano wa mkuu wa mkoa huo, Amos Makalla ambapo wamesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya wachungaji kuwachukua wananchi wanaosumbuliwa na matatizo mbalimbali ili wakatoe ushuhuda kuwa wamepona dhidi ya matatizo yanayowasumbua jambo ambalo ni la uongo na limekua likiipotosha jamii.

Akijibu kero hiyo mkuu wa mkoa wa Mwanza Amos Makalla amekemea tabia hiyo na amewataka wananchi kuzingatia utaratibu za kupata matibabu hospitalini kwani imani za dini hazipaswi kuingilia maelekezo yanayotolewa na wahudumu wa afya hapa nchini.

Aidha Makalla pia amewataka wananchi kuwa makini dhidi ya waganga walioko katika jamii kwani baadhi yao nao wamekuwa ni wapotoshaji na wapo kwa ajili ya kujipatia kipato.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *