Rais wa FIFA, Gianni Infantino ameongeza uwezekano wa kutoa kadi nyekundu kwa wachezaji wanaofunika midomo wanapokabiliana na wapinzani wao wakati wa mtanange katika viwanja vya soka.
Suala hilo la wachezaji kuziba midomo linatarajiwa kuadiliwa mwishoni mwa wiki hii, katika kikao cha Bodi ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (IFAB).
Hili linakuja kufuatia wiki za hivi karibuni, ambapo mchezaji wa Real Madrid, Vinicius Junior alidai kutupiwa maneno ya kibaguzi na mchezaji wa Benfica, Gianluca Prestianni wakati wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hata hivyo, Prestianni alikanusha madai hayo aliyotuhumiwa baada ya kumwendea Vinicius huku akiziba mdomo wake kwa jezi wakati Madrid iliposhinda 1-0 katika mechi ya mkondo wa kwanza wa mchujo.
Prestianni alisimamishwa kwa muda kwa mkondo wa pili, wakati uchunguzi ukiendelea na utaratibu huo kwa ujumla unatarajia huenda ukaanza kutumika katika Kombe la Dunia.