WABUNGE DRC WAONDOA KINGA YA KUSHITAKIWA RAIS MSTAAFU KABILA

Wabunge wa Seneti Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamepitisha uamuzi wa kumwondolea kinga ya mashitaka Rais Mstaafu, Joseph Kabila.

Kabila, ambaye ni Seneta wa maisha wa DRC, anakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo uhaini, uhalifu wa kivita, na uondoaji wa kinga hiyo sasa unatoa taswira ya Kiongozi huyo kuweza kushitakiwa.

Aidha, Kahila pia anatuhumiwa kuunga mkono kundi la waasi la M23, ambalo linahusishwa na kuteka miji kadhaa Mashariki mwa Taifa hilo la Kongo, ikiwemo mji wa Goma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *