Waandishi wa Habari Nchini, wametakiwa kujifunza lugha za kigeni na kujisomea maandiko mbalimbali, ili kuongeza ufanisi katika kazi zao, hasa wanaporipoti taarifa zinapohusu wageni toka nje.
Kamisaa wa Sensa Tanzania Bara, ambaye pia ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda ametoa rai hiyo wakati akifunga mafunzo ya Wanahabari kuhusu usambazaji na matumizi ya matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.
Amesema, uongezaji wa taaluma ni kiungo muhimu cha kusambaza taarifa kwa jamii, huku akiwahakikishia kuwa hakuna Mwandishi atakayekumbwa na matatizo endapo ataandika habari za uchunguzi kwa kufuata ukweli na usahihi.
Mafunzo hayo, yamewahusisha Waandishi wa Habari kutoka Mikoa ya Dodoma na Singida.