Chama kikubwa kabisa cha waandishi habari Ugiriki kimefanya mgomo wa sekta zote za habari kwa saa 24 na katika kipindi hicho televisheni na redio za Ugiriki hazijarusha habari zozote na mitandao ya haikuchapisha habari kwenye tovuti zao, mgomo huo ulitangazwa kuanzia saa kumi na moja kamili Jumanne asubuhi na kumalizika saa kumi na moja kamili asubuhi ya Jumatano.
Muungano huo ulisema unachukua hatua dhidi ya kile ulichokiita mazingira magumu kabisa ya kazi na mishahara ya chini sana ukisema mishahara yao haitoshi kuyakidhi mahitaji ya msingi ya familia na ya kibinafsi na kupanda kwa mfumuko wa bei kumeifanya hali kuwa mbaya zaidi.
Hatua hiyo inajiri kabla ya mgomo wa siku nzima uliopangwa na Muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini Ugiriki, ambao unatarajiwa kuathiri huduma za usafiri wa umma katika kipindi ambacho gazeti la kila wiki la Athens to Vima lilitathmini kuwa bei za bidhaa zimepanda kwa asilimia 37 katika miaka miwili iliyopita.