Na Frank Aman – Geita.
Waajiri katika Sekta mbali mbali ikiwemo Makampuni binafsi yanayojihusisha na Shughuli za Uchimbaji wa Madini wamehimizwa kuweka utaratibu wa kuwajengea uwezo Vijana wanaohitimu katika Fani hizo ili kuweza kuwa uzoefu na Ushindani katika Soko la Ajira hususani katika Fursa za Uchimbaji wa Madini.
Wito huo umetolewa wakati wa kuwatunuku Vyeti Vijana 47 Kati ya 258 waliofanya Vizuri katika Sekta hiyo na kuweza kupata Fursa za Ajira katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) ambapo katika Hafla hiyo Vijana hao pia wamehimiza Makampuni Binafsi kuweka utaratibu wa kuwajengea uwezo wa Kazi hususani wanaohitimu Mafunzo katika Fani mbali mbali ili kuweza kuongeza uwezo wao wa utendani pamoja na kukabiliana na Ushindani katika Soko la Ajira.
Wakizungumza Mwishoni mwa Wiki hii katika hafla ya kuanza kwa Mafunzo Mafupi ya Miezi Sita wa Vijana hao 47 yanayotolewa na Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Dhahabu ya Geita Gold Mine (GGML), baadhi ya Wakuu wa Taasisi za Waajiri na Viongozi wa Mgodi huo wameeeleza namna fursa za ajira zinavyoweza kuwa ni changamoto kutokana na kutokuwa na umahili katika Kazi ambapo pia wamepongeza baadhi ya Makampuni na Taasisi zinazotoa fursa kwa Wahitimu wa ngazi mbali mbali za Elimu kuweza kujijengea uwezo katika Kazi na kuwa na Ushindani katika Soko la Ajira.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Waajiri Tanzania (ATE), Suzan Ndomba amesema kuwa kuwepo kwa Fursa hizo za kuwajengea Uwezo Vijana hususani wanaohitimu Masomo ya Elimu ya juu kutawasaidia kuweza kuwa na Ushindani katika Soko la Ajira na kuweza kunufaika na Fursa hizo ikiwemo zinazotolewa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML).
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela, Mkuu wa Wilaya hiyo, Hashim Komba amehimiza uwepo wa taratibu za kuwajengea uwezo Vijana ambapo itawawezesha kupata Fursa mbali mbali za Ajira.
“Uamuzi uliofanywa na Kampuni ya GGML wa kutoa Mafunzo kwa baadhi ya Wahitimu wa Fani mbali mbali zinazojihusisha na Sekta ya Madini utawawezesha kuwajengea uwezo na kuweza kuwa na Ushindani katika Soko la Ajira,” amesema.
Kwa upande wao, Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Geita (GGML), imeeleza mikakati iliyopo ya kuwainua Vijana hao na kuwawezesha kupata Fursa za Ajira katika Mgodi huo ambapo Charles Masoud ambaye ni Kaimu Rasilimali Watu wa GGML ameelezea mikakati waliyonayo katika kuwainua Vijana waliohitimu Mafunzo hayo ambapo amesema kuwa Asilimia kubwa ya Waajiriwa wa Kampuni hiyo walipitia mfumo huo wa Mafunzo uliowasaidia kuwajengea uwezo wa kiutendaji.
“Lengo letu ni kuwawezesha Vijana waweze kunufaika na Ajira zinazotolewa na GGML namahali mwingine ambapo Asilimia kubwa ya Watumishi wetu wamepitia pia katika mfumo huo na wakanufaika na Ajira pia,” amesema.