Waacheni wasichana wasome

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wakazi wa Mkoa wa Mtwara, kusimama kikamilifu kuhakikisha watoto wa kike wanasoma na kuwaweka mbali na mambo yasiyofaa.

Akizungumza wilayani Nanyamba leo Septemba 16, katika ziara yake mkoani humo, Rais Samia amesema, “Niwaombe sana waachieni wasichana wasome, shule ile ya wasichana ni maalum kwa wenye vipaji vya sayansi huko ndiko tutakapata walimu, madaktari, wahandisi na wataalam katika fani mbalimbali.”

Rais Samia amesema Serikali inajenga shule za sekondari za wasichana za sayansi kila mkoa, hivyo ni muhimu kuhakikisha wanapatikana wasichana wa kusoma kwenye shule hizo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *