Vyakula vya kula wakati wa kufungulia

Kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani ni moja ya jambo ambalo linawawezesha Waislamu kujiweka karibu na kuimarisha imani yao na Mungu.

Kwa mujibu wa maandiko ya Quran tukufu, kufunga mwezi wa Ramadhani ni moja kati ya nguzo kuu tano za Uislamu ambazo kila muumini hutakiwa kuzitimiza katika maisha yake.

Wapo wanaofungulia kwa vyakula vyepesi kama chai, uji au maziwa lakini pia wapo wale wanaofungulia kwa vyakula vizito pasipo kujua madhara yake kiafya.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) vipo vyakula vinavyofaa na visivyofaa kuliwa wakati wa kufungulia katika msimu huu wa Ramadhan ikiwemo vyakula vyenye chumvi nyingi.

TFNC inasema vyakula vyenye chumvi nyingi vinaweza kukausha maji maji mwilini na kumsababishia mtu kiu zaidi ya maji na hivyo kushindwa kufunga siku inayofuata.

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya na lishe, inashauriwa kula vyakula vyepesi wakati wa kufungulia na si vigumu, kwa sababu vyakula vigumu husababisha matatizo mbalimbali ya kiafya.

Vyakula vyepesi unavyoweza kutumia wakati wa kufungulia ni pamoja na tambi, supu, mtori na vinywaji kama uji, chai au maziwa.

Chanzo: Jiko Pont

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *