Vidonda vya tumbo ni vidonda vinavyotokea kwenye ukuta wa tumbo. Vidonda vya tumbo vinajulikana kwa kitaalamu kama peptic ulcers.
Vidonda hivi hutokea kutokana na mashambulizi ya bakteria wanaoitwa Helicobacter pylori (H.pylori) au kulika kwa ukuta wa tumbo kunakotokana na athari za tindikali zilizopo tumboni (Hydrochloric Acid).

Wagonjwa wa vidonda vya tumbo wanashauriwa kula mafuta yatokanayo na samaki ambayo kitaalamu huitwa Omega-3 Fats ambayo yameonekana kutoa ahueni kwa wagonjwa. Kwa mtu ambaye si mgonjwa wa vidonda vya tumbo akila mafuta hayo atakuwa anajiwekea kinga dhidi ya vidonda vya tumbo na magonjwa mengine ya tumbo.
Ulaji wa vyakula vyenye madini na vitamini kwa wingi husaidia pia kuleta ahueni kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo na kutoa kinga kwa wale ambao hawajaathirika. Wenye vidonda vya tumbo wanashauriwa kupenda kula matunda na mboga za majani kama vile karoti, juisi ya kabeji, ndizi mbivu na matunda mengine yenye vitamini C, hali kadhalika maziwa ya mbuzi, jibini na cream za maziwa, kwani huleta ahueni kwa wagonjwa hao.
Sigara ni mbaya kwani huongeza hatari ya mtu kupatwa na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na wasiwasi. Kuepukana na maradhi hayo, watu wazingatie ulaji sahihi ili waweze kuishi maisha ya furaha.
2 responses to “Vyakula vya kula mgonjwa wa vidonda vya tumbo”
Hongera
I think @globalpublisher.co.tz
Copied some context from this without even acknowledge you
That is what we call plagiarism