Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Vladmir Putin Meza Moja na Kim Jong Un

Rais wa Russia Vladimir Putin anatarajiwa kuwasili mjini Pyongyang leo Jumanne Juni 18,2024 katika ziara nadra ambayo inaweza kupelekea kusainiwa mkataba wa ushirikiano wa kimkakati.

Ikielezewa kama ziara ya kiserikali ya kirafiki, ziara hiyo itakuwa ya kwanza kwa Putin kwenda Korea Kaskazini katika kipindi cha miaka 24, huku akitarajia kupata uungwaji mkono katika mashambulizi yake ya kijeshi nchini Ukraine.

Maafisa wa Marekani na Korea Kusini wameishtumu Pyongyang kwa kuipatia Russia zana za kivita, makombora na vifaa vingine vya kijeshi, kama malipo ya kuipa Korea Kaskazini teknolojia muhimu na msaada.

Pande zote Pyongyang na Moscow zilikanusha tuhuma hizo kuhusu msaada wa silaha za Korea Kaskazini kwa Russia,maafisa wa serikali ya Ukraine waliripoti kuhusu ndege zisizokuwa na rubani zilizotengenezwa na Korea Kaskazini, zilizogunduliwa kwenye  mapigano yanayoendelea kati ya pande hizo mbili.

Putin na Kim Jong Un wanatarajiwa kusaini makubaliano mapya ya ushirikiano ambayo yatajumuisha masuala ya usalama, kulingana na mshauri wa sera ya kigeni ya Russia Yuri Ushakov.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *