
Rais Vladimir Putin ameshinda kwa kishindo na kuweka rekodi katika uchaguzi wa urusi uliomalizika siku ya jumapili, huku akiimarisha madaraka yake. Matokeo ya awali yanaonesha kuwa amepata asilimia 87.8 ya kura.
Akihutubia baada ya kumalizika kwa zoezi la upigaji kura Putin amesema, matokeo hayo yanapaswa kutuma ujumbe kwa mataifa ya magharibi kwamba viongozi wake watalazimika kuitiambua urusi yenye ujasiri, iwe ni katika vita ama kwenye amani kwa miaka mingi ijayo.
Kwa matokeo hayo yanayompa ushindi wa kishindo putin mwenye umri wa miaka 71, anatazamiwa kuanza muhula mpya wa miaka sita utakaomfanya ampiku Josef Stalin na kuwa kiongozi wa muda mrefu zaidi wa Urusi kwa zaidi ya miaka 200 iwapo atamaliza muhula wake.
Mataifa ya Marekani, Ujerumani, Uingereza na mengine yamesema kuwa uchuguzi huo haukuwa huru na haki kutokana na kufungwa kwa wanasiasa wa upinzani na kudhibitiwa.