VITUO VYA KULEA WATOTO WADOGO VYATAKIWA KUFUATA UTARATIBU

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

Vituo vya Kulea Watoto wadogo mchana  Mkoani Shinyanga, vimetakiwa kuwa na usajili  na kufuata utaratibu uliowekwa na mamlaka, ili kuweza kuwalinda Watoto kwa mujibu wa sheria ya watoto  namba 21 ya mwaka 2009.

Agizo hilo, limetolewa na  Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi  wakati akifungua kikao  kilicho husisha wamiliki wa Vituo vya Kulea Watoto mchana katika kuangalia hali ya utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) kuanzia mwezi Januari hadi Juni mwaka 2025.

Aidha, amewapongeza wamiliki wote wa vituo vya kulea Watoto wadogo mchana pamoja na  makao ya Watoto kwa kazi nzuri ambayo wamekuwa wakiifanya ya utoaji wa huduma hiyo.

Akiwasilisha mada juu ya vitendo vya  kuzia na kupambana na vitendo vya rushwa  katika kikao hicho, Afisa kutoka Taasisi  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga, Mohamed Doo amesema Serikali itaendelea  kuimarisha mifumo  mizuri  na kuziba mianya ya utoaji rushwa kwa kuhakikisha unakuwepo uimara thabiti.

Doo  amesema Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM)  ni nzuri na  imewaleta wadau pamoja lakini suala la kukemea vitendo vya rushwa watoto wadogo  waanze kufundishwa  kupitia nyimbo nzuri zenye maudhui ya kupinga.

Amesema, watu wamejenga desturi ya kuhalalisha rushwa, ili apate kitu kwa urahisi nakujaribu kutumia njia ya mkato na ushawishi  kwa lengonla kupata kile walichokusudia na jamii kukubali pasipo kutoa taarifa kwenye mamlaka.

“Tumekuwa tukishtaki  watuhumiwa wanaoendesha  vitendo vya rushwa  kwa watumishi wa  taasisi za serikali na taasisi binafsi kwani watu wanajihusisha   wanapobainika wanachukuliwa hatua,” amesema Doo.

Ameongeza kuwa, “sisi tunapokea taarifa nyingi kutoka maeneo tofauti tofauti kwani  zipo baadhi ya  familia zinazotoa hongo ili watoto wao waliopo kwenye vituo walelewe vizuri zaidi kuliko wengine kwa  kufanya hivyo hutamjenga  itaonyesha kubaguliwa au kujibagua kwa  mtoto mwenyewe  nakujiona mnyonge.”

Aidha, alisema zipo rushwa zinazotolewa kwenye vituo kama misaada hasa kwa Watoto wanaolelewa kwenye  makao na vituo  kwa   malengo yao na mbinu hizo zimekuwa zikitumika kuleta  maadili yasiyofaa kwa watoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *