VIONGOZI WATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KUPAMBANA NA RUSHWA.

Frank Aman Geita

Viongozi wa Taasisi za Umma na Binafsi wamekumbushwa kutimiza Wajibu wao katika nafasi walizopata na kuwa Mstari wa mbele katika Mapambano dhidi ya Rushwa kwa kuwa moja ya wajibu wa Kiongozi katika Mapambano hayo kwanza kabisa wao wenyewe wasijihusishe na vitendo vya Rushwa katika kipindi cha Utumishi wao.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Geita, James Ruge katika Kikao cha Wadau wa Mapambano dhidi ya Rushwa ambacho kimefanyika Leo kwa Siku ya pili Mkoani Geita ikiwa na Lengo la kujadili pamoja na wadau na kuwa na Mikakati ya pamoja Kati ya Sekta Binafsi na za Umma katika Mapambano dhidi ya Rushwa Nchini.

Ruge amesema Rushwa ni Dhambi kwa mujibu wa maandiko matakatifu hivyo Viongozi na Watumishi wa Umma wana wajibu wa kushughulikia rushwa kwa kuzingatia kuwa hata Imani zao walizonazo zinapingana na Vitendo hivyo, hivyo Wana Wajibu wa kuwasimamia Watumishi wao.

Akifungua Warsha hiyo ikiwa ni Siku yake ya Pili tangu kuanza kwake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Mohamed Gombati amesema kuwa Semina hiyo na Mafunzo hayo yatasaidia kuwa na Mikakati ya pamoja katika kuzuia Rushwa ambapo ameeleza kuwa changamoto ya Rushwa katika Taasisi yetote inayoendeshwa kwa Misingi ya Rushwa, Uchumi wake hudhoofika kutokana na kukosekana kwa namna Bora ya kuzuia Vitendo hivyo ambayo vimeendelea kuleta athari kubwa kwa Jamii.

Gombati ameeleza kuwa kutokana na kukithiri kwa Vitendo hivyo ndani ya Jamii, Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Geita Gold Mine Limited (GGML) iliamua kuendesha Semina na Mafunzo Maalumu kwa Wadau mbali mbali wakiwemo Watumishi wa Serikali na Sekta Binafsi ili kujadili na kuwepo na Mikakati ya pamoja ya Mapambano dhidi ya Rushwa.

Nao baadhi ya Wadau wa Mkutano huo akiwemo Wakili Msomi Denis Mbekayo ambaye ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Takukuru Nchini ameeleza kuwa wameamua kutoa Semina hiyo ya Mapambano dhidi ya Rushwa kwa kuwa Mkoa huo ni kielelezo kwenye Uwekezaji Nchini Tanzania.

Naye Gilbert Mworia ambaye ni Meneja Mwandamizi wa GGML, Kitengo cha Uendelezaji amesema kuwa Kampuni yao imeweka Mikakati ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ambapo Kampuni hiyo ina Sheria ya kubana Watumishi wao kwa kiasi kikubwa hususani inapohusiana na Vitendo vya Rushwa.

Ameeleza kuwa kwa upande wa Kampuni hiyo, inapobainika Mtumishi wao amejihusisha na Vitendo vya kuomba au kupokea Rushwa wanachukua hatua Kali dhidi yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *