VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUHUBIRI AMANI KUELEKEA KIPINDI CHA UCHAGUZI MKUU 

Na Daniel Gahu, Tanganyika – Katavi.

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika iliyopo Mkoani Katavi, Onesmo Buswelu amewataka Viongozi wa Dini kuhubiri amani, hata katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 2025.

Akizungumza katika kikao hicho kilicho wakutanisha wakuu wa dini wa madhehebu mbalimbali pamoja na wakuu wa taasisi za afya, TAKUKURU, Ustawi wa Jamii, Afya, ulinzi na usalama amebainisha kuwa viongozi wa dini ni nguzo muhimu ambao wako karibu na wananchi hivyo inawapasa kuwahimiza waumini wao juu ya kutenda matendo yaliyomema.

“Wenzetu wa nchi jirani Kuna waumini waliuawa wakiwa katika nyumba ya ibada Kwasababu ya kutokuwa na amani hivyo yawapasa kutoa elimu na mafundisho juu ya umuhimu wa amani,” amesema DC Buswelu

Akiendelea kuzungumza mbele ya viongozi wa dini, Buswelu pia amewataka wakuu hao wa dini kuwaelekeza waumini wao umuhimu wakuwa na afya bora, Kwa kula vyakula vyenye lishe ambavyo vinashauriwa na wataalamu wa afya.

“Ili tuwe na waumini wenye utimamu wa akili ni lazima watumie lishe Bora, wafundishwe, waelimishwe wale nini, kwani msipo fanya hivyo mtakuwa na waumini wenye udumavu kwasabbu sisi wenye sauti ya kuwaambia tumekaa kimya. Tumetengeneza jukwaa hili kwakuongeza wawakilishi wengi katika Kila kata Kwa kutekeleza mpango kabambee unaoongozwa na Mkuu wa mkoa Mheshimiwa Mwanamvua Mrindoko kuwa na wananchi wenye lishe bora ” amesema DC Buswelu.

Kwa upande wake mkuu wa Shirika la kupambana na kuzuia rushwa (TAKUKURU) Bwana Kichele Chacha Mwita amewataka viongozi wa dini kukemea Vitendo vyote vinavyoashiria utoaji na upokeaji wa rushwa Kwa waumini kwani ni chanzo Cha upofu wa kiimani.

“Nafasi ya viongozi wa dini kwanini mko hapa nikwasababu hawa watia nia wa kipindi Cha uchaguzi ni waumini wenu wanakuja makanisani na misikitini wakihitaji labda kuwa mawakala wao au wanakuja kutoa michango mbalimbali kipindi hiki Cha uchaguzi wakati siku za nyuma hawakuwahi kufanya hivyo na wanajiamini kabisa kuwa wewe ukisema inakuwa hivyo kwasababu wewe ukisema ndio sauti ya Mungu yenyewe” amesema Bwana Mwita 

Aidha Kwa upande wake afisa Ustawi wa jamii wa halmashauri ya wilaya ya Tanganyika Bi. Agnes Shauri ameelezea kuwa wilaya ya Tanganyika inakabiliwa na matukio ya Vitendo vya ulawiti na ubakaji takribani arobaini na saba (47) ambapo ni takwimu za mwezi January hadi machi 2025 ambapo inaripotiwa matukio hayo ya ulawiti yamefanywa na madereva Bodaboda pamoja na madereva wa bajaji na hatua za kisheria Bado zinaendelea kuchukuliwa na vyombo vya usalama.

Na kwa upande wa viongozi hao wa dini wakitoa michango na maoni yao, wamemshukuru DC Onesmo Buswelu kwa maono yaki Mungu  yakuwakutanisha viongozi hao kwani ni ishara ya kuthamini na kuheshimu uwepo wa dini katika halmashauri ya Tanganyika.

Aidha, ameahidi pia kuwa watakemea Vitendo vya baadhi ya viongozi wa Serikali kutembea na wake za watu Kwa kiburi Cha kuwa na nguvu ya kifedha na mamlaka kwani ni haramu mbele ya Mwenyezi Mungu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *