Viongozi wa dini pingeni mapenzi ya jinsia moja

Waziri Mkuu Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania, Kassim Majaliwa Amewataka Viongozi Wa Dini Nchini Kuendelea Kukemea Vitendo Vyote Ambavyo Vinapelekea Kuwepo Kwa Tabia Ya Watu Hapa Nchini Kujihusisha Na Mapenzi Ya Jinsia Moja.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Ameyasema Hayo Leo Wakati Akihutubia Umma Kwenye Baraza La Sikukuu Ya Eid El Adh’haa Ambayo Imefanyika Kitaifa Jijini Dar Es Salaam Katika Msikiti Mkuu Wa Mfalme Mohamed Wa Sita, Ulioko Kinondoni.

Majaliwa Amesema Vitendo Hivyo Havikubaliki Kabisa Kwa sababu Vinaenda Kinyume Na Misingi Ya Dini Zetu Lakini Pia Vinadhalilisha Utu Wa Mtu.

Aidha, Waziri Mkuu Ameendelea Kuwasisitiza Viongozi Wa Dini Kuhakikisha Kwamba Wanatumia Ushawishi Walio Nao Kwenye Jamii Kwa Kuendelea Kutoa Matamko Mbalimbali Ambayo Yanakemea Vikali Vitendo Hivyo Vya Watu Kujihusisha Na Mapenzi Ya Jinsi Moja Kwani Ni Kinyume Na Tamaduni Na Desturi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *